Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu amempongeza Dokta Haidari Shimri kwa kupewa madaraka ya urais wa Wakfu-Shia

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar na ujumbe aliofuatana nao, ulio husisha wajumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya na baadhi ya marais wa vitengo kwa Ataba, wamempongeza dokta Haidari Shimri kwa kuteuliwa kuwa rais wa Wakfu-Shia, pongezi hizo amezitoa katika ziara rasmi iliyofanywa siku ya Jumanne Alasiri (28 Dhulhijjah 1441h) sawa na tarehe (18 Agosti 2020m) katika Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya kufanya ziara kwenye malalo ya Maimamu wawili Aljawadaini (a.s).

Sayyid Ashiqar akafikisha salamu za kiongozo mkuu kisheria wa Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na akamtakia mafanikio mema katika kutekeleza majukumu yake na kukamilisha safari ya kutumikia Ataba na Mazaru takatifu pamoja na mazuwaru.

Aidha wamejadili kuhusu miradi mikubwa ya ujenzi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu na shughuli zinazo fanywa katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya Korona, ikiwa ni pamoja na kusaidia sekta ya afya kupambana na maambukizi ya virusi hivyo, sambamba na hatua zilizo chukuliwa kuwalinda mazuwaru pamoja na watumishi dhidi ya maambukizi.

Dokta Shimri amepongeza ziara hiyo na akaonyesha kufurahishwa nayo, naye amewatakia na kuwatumia salamu wafanyakazi wote wa Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria, kwa utendaji uliotukika unaofaa kushukuriwa na kupongezwa.

Ugeni ukakabidhi zawadi kutoka kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awawafikishe wote katika kazi hizi takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: