Kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi kimeratibu nadwa kuhusu turathi (mali-kale) za Karbala na nafasi ya taasisi katika kuzihifadhi

Maoni katika picha
Kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeratibu nadwa kuhusu: (turathi za Karbala na nafasi ya taasisi za kitamaduni katika kuzihifadhi na kuzihuisha), hii ni miongoni mwa nadwa muhimu kutokana na nafasi ya mji wa Karbala kihistoria, kufuatia uwepo wa Ataba takatifu na mazaru tukufu katika mji huu, pamoja na shule za dini na maktaba binafsi na za umma, nadwa hiyo itafanywa siku ya Alkhamisi tarehe (20 Agosti 2020m) kupitia jukwaa la (GOOLE MEET) saa kumi na moja Alasiri.

Mkuu wa kituo Ustadh Swalahu Siraaj ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu nadwa hiyo, amesema: “Hii ni nadwa ya pili kufanywa na kituo kwa njia ya mtandao, ambayo watu wanashiriki wakiwa mbali (kwa njia ya masafa), kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona imelazimika kutumia majukwaa ya kimtandao kuendeleza harakati, nadwa itakuwa na mihadhara miwili:

Kwanza: nafasi ya kituo katika kupiga picha na kuandaa faharasi za nakala-kale kwa njia ya mtandao kwenye maktaba binafsi na za umma na umuhimu wake kielimu, mada hiyo itawasilishwa na mtafiti Haidari Jaasim Kinani mtaalam wa faharasi za nakala-kale katika kituo.

Pili: turathi za Karbala zisizo hakikiwa, itawasilishwa na mkufunzi Mustwafa Twaariq Shibliy. Washiriki watatumiwa vyeti vya ushiriki kwenye barua pepe zao”.

Akamaliza kwa kusema: Tunamkaribisha yeyeto anayetaka kushiriki katika walimu na watafiti, ajiunge kupitia link ifuatayo: https://meet.google.com/vgc-oooa-tto

katika muda uliotajwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: