Wasimamizi wa haram tukufu: Huduma zetu zinaendelea pamoja na kuwepo janga la Korona

Maoni katika picha
Kiongozi wa idara ya kusimamia haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) bwana Nizaar ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa idara yetu wanafanya kazi muda wote pamoja na kuwepo kwa janga la Korona, wanafanya kazi ya utowaji wa huduma na za afya, kwa ajili ya kuhakikisha mazingira yanakuwa salama na tulivu”.

Akaongeza kuwa: “Watumishi wetu wanajukumu la kutoa huduma katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kwenye eneo la pambo la dhahabu (sega la dhahabu) lililopo upande wa Kibla, wanasimamia na kuongoza watu wanao ingia na kutoka wakati wote, kwenye ziara za kawaida na zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ili kuondoa msongamano na kurahisisha mjongeo ndani na nje ya haram, aidha wanawajibika kusafisha wakati wote kila sehemu, kuanzia kwenye dirisha la kaburi, sakafu ya haram na korido zake, bila kusahau kuta, mapambo, milango, taa, viyoyozi na kila kitu kilichopo katika eneo la haram”.

Akabainisha kuwa: “Katika mazingira ya kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Korona kazi zetu zinaendelea kama kawaida, bali imeongezeka kazi ya kupuliza dawa kila wakati kwenye maeneo yote ya haram takatifu, pamoja na kuweka vitakasa mikono katika milango yote, sambamba na kuzingatia kazuni zote za afya zilizo pasishwa na idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ndani ya kipindi hiki tumefanya kazi nyingi ambazo ilikuwa ni vigumu kuzifanya au zilikua zinachukuwa muda mrefu kukamilika siku za nyuma kutokana na wingi wa mazuwaru, tambua kuwa kazi hizi tunazungumzia upande wa wanaume, kuna kazi sawa na hizi pia hufanywa na dada zetu wa Zainabiyaat upande wa wanawake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: