Kumaliza kuweka mapambo yanayo ashiria huzuni katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya wamemaliza kuweka mapambo yanayo ashiria huzuni za Ashura kwenye korido zake, ndani na nje ya haram kuna mapambo meusi, kama sehemu ya kuupokea mwezi wa Muharam na kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na maswahaba wake.

Makamo rais wa kitengo cha mapambo Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Baada ya idara ya ushonaji kumaliza kushona mabambo ya huzuni, watumishi wa kitengo chetu walianza kazi ya kuyaweka kwenyo korido na kuta za Ataba ya mbeba bendera ya Twafu Abulfadhil Abbasi (a.s), walianza kazi hiyo kwa zaidi ya siku tatu zilizo pita, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu leo tumemaliza kazi hiyo, tulianza kwa kupamba ukuta wa haram tukufu, nguzo na ukuta unaozunguka haram kwa nje, tumeweka vitambaa na mabango meusi yenye nakshi na jumbe mbalimbali zinazo ashiria huzuni sehemu zote hadi kwenye milango ya haram takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Vitambaa vimeandikwa kwa umaridadi mkubwa na vimedariziwa kwa uzi mwekundu, vinaujumbe wa kauli za maimamu (a.s) kuhusu Imamu Hussein (a.s) na ndugu yake (a.s), kuna sehemu maalum iliyo andikwa majina ya bibi Zainabu na Ummul-Banina (a.s) pamoja na Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Kumbuka kuwa mapambo yanawekwa kitaalamu kwa kutumia gundi maalum isiyo haribu sehemu inayo bandikwa, na unaweza kuondoa kwa urahisi baada ya kumaliza maombolezo, baada ya mwezi wa Muharam na Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: