Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi ya Ashura chini ya utekelezaji wa masharti ya kujikinga na maambukizi

Maoni katika picha
Katika mazingira ya huzuni na majonzi ya msiba wa bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s), kama ilivyo katika kila mwaka, Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi jirani na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake (a.s), chini ya utekelezaji wa kanuni za afya na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu.

Mjumbe wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Jawadi Hasanawi amesema kuwa: “Atabatu Abbasiyya imezowea kufanya majlisi za kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nymbani kwake pamoja na wafuasi wake kwa aina mbalimbali za uombolezaji kila mwaka, ikiwa ni pamoja na kufanya majlisi ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mwaka huu kutokana na kuwepo tatizo la maambukizi ya virusi vya Korona na kufuata maelekezo ya Marjaa Dini mkuu pamoja na wizara ya afya, majlisi inafanywa karibu na Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye uwanja uliopo mkabala na mlango wa Kibla, na kuhudhuriwa na idadi maalum ya watumishi pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi”.

Akaongeza kuwa: “Mzungumzaji ni Sayyid Hashim Batwaat na zinafanywa kila siku saa kumi na mbili na nusu asubuhi, hadi siku ya mwezi tisa Muharam, anazungumzia harakati ya Imamu Hussein (a.s) na kujitolea kwake kwa ajili ya umma wa kiislamu na ulimwengu kwa ujumla, na jinsi alivyokuwa taa linalo angazia watu huru wa aina tofauti na mitazamo mbalimbali, hakika yeye (a.s) ni nuru ya walimwengu wote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: