Njooni kwenye maombolezo: Dirisha la kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) limewekwa vazi la uombolezaji wa Ashura

Maoni katika picha
Dirisha takatifu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) limewekwa vazi la kuomboleza Ashura, kuonyesha huzuni na majonzi waliyopata Ahlulbait (a.s) katika mwezi huu, kwa kuuwawa mjukuu wa Mtume Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake, katika ratiba ya kuomboleza msiba wa Twafu, vazi hilo limewekwa na watumishi wa haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya.

Vazi limetengenezwa kwa kitambaa cha kifahari na kuandikwa kwenye pande zake nne maneno yafuatayo:

  • - Upande wa mlango wa dirisha takatifu umeandikwa (Ewe mwenye kuhami wasitiri wakina Fatuma), juu yake kuna (ufito wa dhahabu) na chini yake pameandikwa (Amani iwe juu yako ewe mlango wa haja).
  • - Upande wa Kibla umeandikwa (Amani iwe juu yako ewe mja mwema mtiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kwa kiongozi wa waumini na Hassan na Hussein), halafu limefuatia neno lisemalo (Amani iwe juu yako ewe mnyweshaji wenye kiu Karbala).
  • - Upande wa mkabala wake umeandikwa (Amani iwe juu yako ewe mtoto wa waislamu wa kwanza na wakongwe wa Imani na wenye msimamo mkubwa wa Dini ya Mwenyezi Mungu) likifuatia neno lisemalo (Amani iwe juu yako ewe mnyweshaji wenye kiu Karbala).
  • - Upande mwingine wa mlango wa dirisha umeandikwa (Amani iwe juu yako ewe mwezi wa bani Hashim), likifuata neno lisemalo (Amani iwe juu yako ewe mbeba bendera).

Maandishi hayo yanarangi ya njano iliyo zungushiwa ufito wa mapambo.

Huzuni na majonzi yametanda kila sehemu ndani ya haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kuta zake zimewekwa mapambo meusi kama ishara ya kuonyesha huzuni na majonzi katika kumbukumbu ya msiba wa Ashura pamoja na kuweka vitambaa vyeusi kwenye minara ya malalo takatifu, vilivyo andikwa majina ya sifa (laqabu) za Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: