Alama zinazo onyesha uingiaji katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ili kuhakikisha umbali kati ya mtu na mtu

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo kinacho simamia haram tukufu wameweka alama za kuingia ili kuhakikisha unapatikana umbali wa mtu na mtu kwa wale wanaoshiriki kwenye mawakibu za waombolezaji zinazo ingia katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ili kulinda usalama wao na kutekeleza maelekezo ya Marjaa Dini mkuu pamoja na muongozo wa sekta za afya.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu imeshafanya mambo mbalimbali katika kijikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ndani na nje ya haram tukufu, mambo yote imeyafanywa chini ya usimamizi wa idara ya madaktari na kufuata maelekezo ya wizara ya afya, jambo hili ni moja ya sehemu za kulinda usalama wa waombolezaji ambao idadi yao imesha pangwa kwenye kikao cha viongozi wa mawakibu za kuomboleza”.

Akaongeza kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu wameweka alama zinazo onyesha sehemu anayo takiwa kutembea mtu pamoja na kuzingalia umbali baina yao, umbali wa kila alama ni (2sm30) zimechorwa kwa rangi ya njano alama za nyayo mbili na zimeandikwa (simama hapa) kwa lugha ya kiarabu na kiengereza, umbali wa alama ya kusimama mtu na mwingine ni mita moja, na huo ndio umbali uliopangwa na mamlaka husika, alama hizo zimewekwa kwenye milango iliyopangwa kutumika kwa kuingilia mawakibu na zimewekwa kwa gundi imara na zinamuonekano mzuri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: