Vituo vya Ashura.. mwezi pili Muharam kuwasiri msafara ya Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala

Maoni katika picha
Riwaya zinaonyesha kuwa Imamu Hussein (a.s) aliwasiri katika ardhi ya Karbala pamoja na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake mwezi pili Muharam mwaka wa sitini na moja Hijiriyya siku ya Alkhamisi kwa mujibu wa mapokezi mashuhuri, wakiwa wamesongwa na mitihani mingi, waliandamwa na utawala wa kidhalimu uliokuwa umekusudia kumwaga damu zao au kuwalazimisha waishi katika udhalili na unyonge, na Mwenyezi Mungu hataki hilo kwao.

Imamu Hussein (a.s) aliangalia kundi la watu wa nyumbani kwake (a.s) walio katika umri mdogo mwanzoni mwa ujana, akalia sana na akasema: “Ewe Mola hakika familia ya Mtume wako Muhammad (s.a.w.w), tumetolewa na kufukuzwa pamoja na kusumbuliwa katika haram ya babu yetu, bani Umayya wametufanyia uadui, ewe Mola tulipie haki yetu na utunusuru na watu madhalimu”. Kisha akawaambia watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake kuwa: “Watu wanaabudu dunia na Dini imebaki kwenye ndimi zao, wanaifuata pale itakapokuwa na maisha yao wakipata mtihani wanapungua watu wa Dini”.

Maneno hayo matukufu ni ukweli halisi uliopo katika maisha ya watu, wanaabudu dunia zama zote na kila sehemu, Dini haina nafasi katika nyoyo zao, wakipata mtihani huikimbia na kuikataa, hakika alisema kweli Dini imebaki kwenye ndimi zao.

Imamu akawaangalia wafuasi wake na kuwaambia: “Amma baada, Tumefikwa na mnayo yaona, hakika dunia imebadilika na kubaki tupu, haina mema yake, hayakubaki ispokua sawa na unyevunyevu wa maji kwenye chombo, au sawa na jangwa la malisho lisilokuwa na majani, hivi hamuoni haki haifanyiwi kazi na batili haikatazwi, muumini atamani kukutana na Mola wake, hakika mimi sioni kifo ispokuwa ni faraja, na kuishi na madhalimu ni mateso”.

Katika maneno hayo ametaja aina za mitihani na mabalaa, na kwamba dunia imebadilika, imejaa manyanyaso ya aina mbalimbali, lakini mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) hakukata tamaa wala hakurudi nyuma, kwa sababu alikua anaona wazi haki haifanyiwi kazi na batili haikatazwi, alihitaji kuishi kwa heshima au kufa kishahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwake ndio faraja.

Alipomaliza khutuba yake, wafuasi wake wote walimzunguka, nao walionyesha moyo wa pekee katika kujitolea kwa ajili ya kusimamisha Dini na uadilifu, kila mmoja aliongea kwa Imani na ikhlasi, Imamu akawashukuru na kuwasifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: