Kitengo cha usimamizi wa haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya kimemaliza kutabdika zulia jekundu eneo lote la haram linalokadiriwa kuwa mita (5250).
Kwa mujibu wa maelezo ya makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Zainul-Aabidina Qurashi, amesema: “Hakika jambo hili ni makhsusi katika mwezi wa Muharam na sehemu ya kuonyesha huzuni na majonzi, mwanzoni mwa mwezi huu huwa tunatandika busati lekundu kwa ajili ya kulinda sakafu ya haram tukufu, na kurahisisha utembeaji wa mawakibu zinazo ingia kwenye malalo takatifu katika kipindi hiki”.
Akaongeza kuwa: “Tulichukua kapeti kwenye godauni la Ataba tukufu lililopo katika kitongiji cha Ibrahimiyya baada ya kubaini vipimo vinavyo takiwa kutandikwa, kabla ya kutandika tulifunika sakafu kwa nailoni kisha ndio tukatandika zulia eneo lote ya haram takatifu”.
Akasisitiza kuwa: “Kutokana na maelekezo ya kiafya yaliyo tolewa na idara ya madaktari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, tunafanya kazi ya usafi na kupuliza dawa kila wakati tena kwa kutumia vifaa maalum”.