Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) imewekwa mapambo meusi na watumishi wake wanasaidia kuongoza matembezi ya mawakibu za waombolezaji

Maoni katika picha
Maqaam ya Imamu Mahadi (a.s) ni moja ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, kama kawaida unapoingia mwezi wa Muharam kila mwaka huwekwa mapambo meusi kwenye kuta zake na hutangaza maombolezo huku kubba lake likipandishwa bendera ya huzuni.

Rais wa kitengo hicho bwana Adnani Dhaifu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika Maqaam inamambo iliyozowea kuyafanya kila mwaka, hufanya shughuli mbalimbali za uombolezaji, zinazo huisha kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake (r.a), lakini kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa, imelazimika kupunguza shughuli zake kwa kiwango fulani, ili kuendana na mazingira ya afya pamoja na kutekeleza maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na maelezo ya sekta husika, miongoni mwa mambo tuliyo fanya ni kuweka mazingira ya msiba sehemu zote za Maqaam, hadi kwenye sehemu za kumbi zilizo ongezwa sambamba na kufunga taa nyekundu, bila kusahau kupuliza dawa ya kuuwa bakteria kwa ajili ya kujikinga na maambukizi”.

Akaongeza kuwa: “Idara ya ushonaji chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri kilitupa mapambo ya huzuni tuliyo hitaji, ikiwemo bendera ya kubba iliyo badilishwa sambamba na bendera za kubba ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya mwezi mosi Muharam, nayo ni nyeusi aliyo andikwa neno lisemalo (Yaa Qaaimu Aali Muhammad) kwa rangi nyekundu, aidha yamewekwa makundi ya watumishi kusaidia kuongoza matembezi ya mawakibu zinazo pita katika barabara zilizo pembezoni ya Maqaam hiyo, kwa kuzingatia umbali wa mtu na mtu unaotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa idara ya afya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: