Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa mihadhara ya Ashura kwa nyakazi na sehemu tofauti, pamoja na kuzingatia masharti ya afya kama alivyo elekeza Marjaa Dini mkuu na wizara ya afya.
Miongoni mwa mihadhara hiyo, ni ile inayo tolewa kila siku jioni ndani ya ukumbi wa utawala wa Ataba tukufu, na kuhudhuriwa na watumishi wachache wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kukumbushana yaliyojiri kwa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake katika siku kama hizi, mihadhara hii itaendelea kwa muda wa siku tisa, kuanzia usiku wa mwezi mosi Muharam, chini ya uhadhiri wa Sayyid Hashim Batwaat.
Mihadhara inasajiliwa na kurushwa kwenye mitandao mbalimbali ya mawasiliano, anazungumza kuhusu Imamu Hussein (a.s) kuwa ndiye mrithi wa mitume, pamoja na kuzungumzia ziara maalum za Imamu Hussein (a.s) na kujikita katika ziyaratu waarith, hiyo ni ziyara mashuhuri zaidi iliyopokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), pamoja na kuguzia uwelewa uliopo kwenye ziara hiyo.