Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel kimetengeneza masafa maalum ya bure kwa ajili ya kurusha maombolezo ya Ashura kutoka ndani ya makao makuu ya uombolezaji wa Husseiniyya katika mji mtakatifu wa Karbala, na kufikisha sauti yake kila kona ya dunia pamoja na kuonyesha harakati za Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia zaidi ya kamera (55) zilizo fungwa maeneo maalum na zinazo bebwa, zipo ndani na nje ya Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na eneo la katikati ya Ataba hizo.
Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Ahmadi Swadiq amesema kuwa: “Kufuatia mkakati uliowekwa na idara ya kitengo hicho kulingana na mazingira ya kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, tumeandaa masafa ya bure kupitia anuani zifuatazo:
Satellite: Eutelsat 7A at 7.0 East(W3A)
DOWNLINK:12680.200 H
MOD:DVBS2
QPSK
FEC:5/6
Sr :3250
HD/MPEG-4".
Akatoa wito kwa vyombo vyote vya habari vya kitaifa na kimataifa vinavyo penda kurusha maombolezo haya wanaweza kufanya hivyo kupitia anuani hizo, hali kadhalika wanaweza kufuatilia matangazo au kuangalia ratiba kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii ifuatayo:
Youtube
Facebook
Instagram
Twitter
*Link inayo tumika kuchukua vipindi ni*
https://youtu.be/_gOxzD3IAz0
kwa maelezo zaidi piga namba za simu zifuatazo: (+9647706054144 / +9647732407576 / +9647805085858).
Kumbuka kuwa kituo cha kutengeneza vipindi Alkafeel kimepiga hatua kubwa katika kurusha picha zenye ubora mkubwa, kina watumishi mahiri wenye uzowefu mkubwa, wanatumia utaalamu na uzowefu walio nao kurusha bicha bora zaidi, zinazo onyeshwa na makumi ya vyombo vya habari nadi nan je ya Iraq.