Taasisi ya kimataifa ya madaktari Al-Imamiyya inatoa huduma za matibabu kwa njia ya masafa kufidia huduma ambazo hutoa kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Taasisi ya kimataifa ya madaktari Al-Imamiyya (IMI) kwa miaka zaidi ya tisa imezowea kuwapa huduma ya matibabu mazuwaru kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, hujenga mahema ambayo huwa na madakdari bingwa wa maradhi tofauti kutoka kila sehemu ya dunia.

Mwaka huu taasisi imebadilisha namna ya utowaji wa huduma, inatumia njia ya kutoa huduma kwa njia ya masafa, kwa ajili ya kupunguza msongamano wa watu kutokana na kuwepo kwa janga la Korona, imetoa vifaa-tiba kwa taasisi za afya ili kuzisaidia kupambana na janga la Korona.

Kiongozi wa idara ya tiba katika Atabatu Abbasiyya na muwakilishi wa taasisi hiyo (IMI) hapa Iraq Dokta Osama Abdulhussein amesema kuwa: “Hakika taasisi ya kimataifa ya madaktari Al-Imamiyya imesajiliwa na umoja wa mataifa, inawanachama zaidi ya elfu kumi kutoka nchi zaidi ya (12), imekuwa ikishiriki kutoa huduma za afya hapa Iraq kwa miaka mingi, mwaka huu imebadilisha utaratibu wa kutoa huduma kwa mazuwaru, na kuamua kutoa vifaa-tiba kwa taasisi za afya kutokana na tatizo la janga la Korona”.

Akabainisha kuwa: “Miongoni mwa vifaa hivyo ni mavazi ya kujikinga na maambukizi waliyo toa kwa kushirikiana na taasisi ya bibi Fatuma -a.s- (LFCT) pamoja na barakoa na vifaa vingine”.

Kumbuka kuwa taasisi hiyo hujenga mahema ya kutolea huduma za matibabu kwa mazuwaru kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya kila mwaka katika kipindi cha miaka tisa mfululizo, chini ya madaktari kutoka nchi tofauti duniani kama vile (Uingereza, Marekani, Ailend, Tanzania…), hutoa huduma saa ishirini na nne, mwaka jana idadi ya madaktari wa kujitolea ilifika (120).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: