Vituo vya Ashura: Mwezi sita Muharam Habibu bun Mudhahiri awaomba bani Asadi waende kumnusuru Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Riwaya zinaonyesha kuwa mwezi sita Muharam mwaka 61h, baada ya Habibu bun Mudhahiri kuona wingi wa askari wanaotaka kupigana vita na Imamu Hussein (a.s), alimfuata Imamu (a.s) na akamuambia: Bwana wangu! Maeneo haya kuna kitongoji cha bani Asadi, unaniruhusu niende kuwaita waje kukunusuru? Hussein (a.s) akamuambia: Ndio nakuruhusu, nenda. Katikati ya usiku Habibu akaenda kwenye kitongoji kile, wakazi wakamkaribisha vizuri, wakamuuliza: Unashida gani? Akasema: Mimi nimekuleteeni jambo jema ambalo halijapata kuletwa na mtu yeyote, nimekuja kukuiteni twende kumnusuru mtoto wa binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), ibun Saadi amemzunguka na jeshi, na nyie ni watu wa ukoo wangu nitiini mtapata utukufu duniani na akhera, yeyote atakaeuwawa miongoni mwenu atakuwa rafiki wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) siku ya kiyama.

Bwana mmoja anaitwa Abdullahi bun Bashiri akasema: Ewe Habibu mimi ni mtu wa kwanza ninaeitikia wito huu, na nitaenda pamoja na wewe. Anasema: wakaendelea kujitokeza hadi wakafika watu tisini, wakatoka pamoja nae kwenda kwa Hussein (a.s).

Anasema: Akatoka mtu katika kitongoji hicho akaenda kumuambia ibun Saadi tukio hilo, Omari bun Saadi akamwita Azraq Shami, akampa wanajeshi mia tano wapanda farasi wakaenda kuwavizia pembeni ya mto Furaat, Bani Asadi wakakutana ghafla na jeshi kubwa la wapanda farasi, Habibu alipo muona Azraq akapiga ukulele kwa kusema: Ole wako ewe Azraq.. acha tuzuwiwe na asiyekuwa wewe.

Akasema: Bani Asadi walipoona hawana uwezo wa kupigana na jeshi hilo wakarudi majumbani mwao, Habibu akabaki peke yake, akarudi kwa Hussein (a.s) na akamuambia kilicho tokea, Hussein (a.s) akasema: Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea, na wala hamtataka ispokuwa atake Mwenyezi Mungu, hakuna hila wala nguvu ispokuwa kwa Mwenyezi Mungu mkuu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: