Idara ya elimu katika kitengo cha malezi na elimu ya juu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa semina kwa njia ya mtandao katika kipindi hiki cha janga la Korona, miongoni mwa mafundisho wanayo toa ni namna ya kutumia mitandao pamoja na kusimamia majukwaa ya ufundishaji mitandaoni na inaendelea kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao hiyo wakufunzi.
Ustadh Amiri Saadi kiongozi wa idara ya ufundishaji endelevu katika kitengo cha malezi na elimu amesema kuwa: semina hii inawalenga wakufunzi wa shule za Al-Ameed kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutumia majukwaa ya ufundishaji kwa njia ya mtandao, pamoja na namna ya kuandaa masomo kwenye mtandao yanayo endana na mahitaji ya zama hizi sambamba na ulemwengu wa masomo wa baadae.
Akaongeza kuwa: Semina itaendelea kwa siku kadhaa na itakuwa na sehemu tatu.
Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kimeongeza utendaji wa kufundisha kwa njia ya mtandao ili kunufaika kwa kiwango kikubwa na teknolojia za kisasa.