Kwa upasuaji wa aina yake.. Madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel wamefanikiwa kumfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo la kichwa kikubwa (mgongo wazi)

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kumtibu mtoto aliyekuwa na tatizo la kichwa kikubwa (mgongo wazi).

Daktari bingwa wa upasuaji wa kichwa Dokta Mustwafa Aghakoni amesema kuwa: “Jopo la madaktari chini ya usimamizi wetu limefanikiwa kumfanyia upasuaji mtoto mwenye tatizo la kichwa kikubwa (mgongo wazi) mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi nane”.

Akaongeza kuwa: “Tatizo la kujaa maji kwenye ubongo (mgongo wazi) hutokana na kubana baadhi ya mishiba ya kwenye ubongo”.

Akafafanua kuwa: “Baada ya kufanyiwa upasuaji wa kwanza amefanyiwa upasuaji mwingine wa kurekebisha kichwa na kukifanya kuwa na muonekano wa kawaida, na sasa hivi anaendelea vizuri”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inajitahidi kutoa huduma bora za matibabu wakati wote kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa, chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwenye hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel kila baada ya muda fulani hualika madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kutoka nchi tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa waliopo katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: