Vituo vya Ashura: kuimarika kuzingirwa Imamu Hussein (a.s) na Abulfadhil (a.s) kwenda kuleta maji.. ni miongoni mwa matukio ya mwezi saba Muharam

Maoni katika picha
Kitabu cha Arbaabul-Maqaatil kimeandika kuwa siku ya mwezi saba Muharam mwaka wa 61h, maadui waliimarisha kumzingira Hussein (a.s) pamoja na watu aliokuwa nao, aidha Imamu Hussein na watu wake waliishiwa maji, huku Omari bun Saadi (laana iwe juu yake) akiweka askari mia tano kulinda mto wa Alqami, baada ya kupokea barua kutoka kwa maluuni ibun Ziyaad ikimtaka amzuwie Imamu Hussein (a.s) na watu wake kutumia maji ya mto huo.

Imamu Hussein (a.s) na watu wake wakaanza kuteseka na kiu, watoto wakaanza kulia kiu na kuomba maji mbele ya Abu Abdillahi (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake watiifu, hawakuwa na maji hata kidogo huku baina yao na mto kuna jeshi limesimama na siraha kuwazuwia wasifike mtoni, lakini mnyweshaji wa maji Karbala hakuweza kuvumilia hali hiyo.

Abu Abdillahi alimteua ndugu yake Abbasi (a.s) aende kuchota maji, wakati anateuliwa yeye mwenyewe tayali nafsi yake ilikuwa inamsukuma kufanya hivyo, akampa watu ishirini wakiwa na viriba ishirini vya kuchotea maji, wakaondoka usiku kwenda mtoni kuchota maji bila kuogopa ukubwa wa jeshi linalo linda mto, kwa sababu wameongozana na simba wa watu wa nyumba ya Mtume Abulfadhil Abbasi (a.s), bendera ikabebwa na Naafii bun Hilali Aljamaliy aliyekuwa miongoni mwa hao watu ishirini, Amru bun Hajjaaj akapiga ukelele kwa kusema: Nani wewe? Na unataka nini? Naafii akajibu: Mimi ni Naafii, tumekuja kunywa maji mliyo tuzuwia. Akasema: Kunywa wala usibebe hata kidogo kumpelekea Hussein. Naafii akasema: Hapana, sitakunywa hata tone moja wakati Hussein na watu wake wakiwa na kiu. Naafii akawaambia watu wake: Jazeni maji vyombo vyenu. Watu wa ibun Hajjaaji wakawavamia, baadhi ya watu wakawa wanachota maji na wengine wanapigana, na hapo ndio ushujaa wa mtoto wa simba machachali Abulfadhil Abbasi (a.s) ulipo onekana, aliongoza mapigano hayo na wakafanikiwa kuchota maji na kurudi salama pamoja na maji kwenye mahema ya Imamu Hussein (a.s) na watu wake, watoto wakapewa maji yale na kupoza kiu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: