Kutangaza majina ya washindi wa shindano la (Safinatu Najaa) lililo endeshwa kwa njia ya mtandao la mashairi faswaha ya wanafunzi wa vyuo

Maoni katika picha
Idara ya uhusiano wa vyuo na shule chini ya kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza majina ya washindi wa shindano la (Safinatu Najaa) lililo endeshwa kwa njia ya mtandao la mashairi faswaha, lililofanywa na wanafunzi wa vyuo mwishoni mwa mwezi uliopita, nalo ni sehemu ya harakati zilizo fanywa ndani ya kipindi hiki, kama sehemu ya kuendelea na harakati zake bila kusimama wakati huu wa kipindi cha janga la Korona.

Rais wa kamati ya majaji wa shindano hilo, Dokta Sarhani Jafaat Salmani ambae ni rais wa kitenge cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu amesema kuwa: “Mashairi yaliyo wasilishwa kwenye kamati ya majaji yalipimwa kwa kuangalia vigezo vingi, tuliangalia sauti, muundo wa shairi, mtazamo wake kifikra, lugha ya kishairi na usahihi wa maneno”.

Akaongeza kuwa: “Washindi wa shindano hilo ni:

Mshindi wa kwanza: Muhammad Ghazi Suani Alhusseiniy kutoka chuo kikuu cha Mosul/ kaswida yake isemayo (Alqami ya kiu cha Hussein).

Mshindi wa pili: Amiru Twaha Abdullahi Swabihawi kutoka chuo kikuu cha Karbala/ kaswida yake isemayo (Wahaju fi Aakhiri Darbi).

Mshindi wa tatu: Habibu Muqbil Atwiyya kutoka chuo kikuu cha Waasit/ kaswida yake isemayo (Munajaat).

Kiongozi wa harakati za chuo Ustadh Muntadhir Swafi amesema kuwa: “Wazo la shindano hili limetokana na lengo la kuandika kitabu cha mashairi kuhusu nafasi ya Imamu Hussein (a.s) mbele ya Mwenyezi Mungu na kumuomba Allah atuondolee mabalaa na maradhi, pamoja na kubaini vipaji vya usomaji wa mashairi, sambamba na kuendeleza uwezo wa vijana katika mazingira haya magumu, idadi kubwa ya wanafunzi wa chuo imeshiriki kwenye mashindano haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: