Mawakibu za kudoa huduma chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia idara zake zilizopo kwenye mikoa tofauti, zinahudumia waombolezaji wa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na wafuasi wake chini ya mfumo wa kujikinga na maambukizi.
Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Qassim Rahim Maámuri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kwakua mwezi wa huzuni mwaka huu umekuja wakati wa maambukizi ya virusi vya Korona, mawakibu zilizo chini yetu zimejipanga kutoa huduma chini ya mfumo madhubuti wa kujikinga na maambukizi”.
Akaongeza kuwa: “Miongoni mwa mambo yanayo fanywa na mawakibu ni kupuliza dawa sehemu zote zinazo fanywa vikao (majlisi) za kuomboleza, pamoja na kugawa barakoa na vitakasa mikono, yote hayo yanafanywa kwa kushirikiana na kamati maalum ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona”.
Kumbuka kuwa idara ya ustawi wa jamii pamoja na ofisi zilizo chini yake zimefanya kazi kubwa ya kugawa chakula na kupuliza dawa kwenye majengo ya serikali na taasisi za umma na binafsi pamoja na mitaa ya makazi ya watu tangu lilipo tangazwa janga la virusi vya Korona hadi sasa, na kazi hii ni muendelezo wa juhudi hizo.