Atabatu Abbasiyya tukufu imejenga kituo cha kugawa maji safi kwenye mitaa mitatu ya Karbala

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu miongoni mwa miradi yake imetengeneza kituo kamili cha kusafisha maji (R.O) katika mtaa wa Mulhaq, Hussein (a.s) na Bahadaliyya, kwa ajili ya kupunguza tatizo la maji kwa wakazi wa mitaa hiyo, nacho ni moja ya vituo vingi vilivyo anzishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mradi huu ni sehemu ya miradi mingi inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kusaidia taasisi mbalimbali, pamoja na kutoa misaada tofauti kwenye vitongoji mbalimbali, watumishi wa idara ya ufundi chini ya kitengo cha maji wamejenga kituo cha kusafisha maji (R.0) chenye ujazo wa lita 10,000”.

Akaongeza kuwa: “Kituo chenye ukubwa huo kinaweza kuhudumia nyumba (1000) za mtaa wa Mulhaqu na mtaa wa Hussein (a.s) pamoja na kitongoji cha Bahadaliyya, mradi huo pia unahudumia karibu nyumba (1000) pamoja na kituo cha Hashdu-Shaábi kwa kusambaza maji kwa kutumia gari maalum za maji”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeshajenga miradi mingi ya kutoa huduma, miongoni mwa miradi hiyo ipo inayo husiana na maisha ya mwananchi moja kwa moja, imejitahidi kupunguza changamato za raia kadri ya uwezo wake, miongoni mwa changamoto kubwa inayopewa kipaombele ni changamoto ya tatizo la maji, imejenga vituo vingi vya kusafisha na kusambaza maji (R.O station) sehemu mbalimbali, wanufaika wa miradi hiyo ni maelfu kwa maelu ya watu pamoja na wakulima na mawakibu, kuna vituo rasmi vilivyo anzishwa kwa ajili ya kuhudumia wakulima na mawakibu ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: