Kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu kinafanya usafi na kupuliza dawa

Maoni katika picha
Miongoni mwa kazi zake za utumishi katika mwezi mtukufu wa Muharam, kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili tukufu kinafanya usafi na kupuliza dawa kwenye eneo hilo takatifu la katikati ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na sehemu iliyowekwa paa, bila kusahau barabara za pembezoni mwake na vituo vya kutolea huduma.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi amesema kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu wanafanya kazi mfululizo mwaka mzima, kuna msimu huwa na kazi nyingi, nao ni msimu wa kipindi cha huzuni za Ahlulbait (a.s) mwezi mtukufu wa Muharam, tumeweka mkakati maalum wa kudumisha usafi na kupuliza dawa”.

Akaongeza kuwa: “Opresheni hii inafanywa na idara ya usafi, na haiishii kufanya usafi pekeyake, bali tunapuza dawa kwa ajili ya kuwalinda mazuwaru watukufu na watumishi dhidi ya maambukizi ya virusi vya Korona, kazi hiyo inafanywa kwa kufuata maelekezo ya Atabatu Abbasiyya na kamati maalum ya kupambana na janga la Korona”.

Akasema: “Pamoja na maelekezo ya afya yaliyo tolewa na idara ya madaktari wa Ataba, tumechukua tahadhari zote za kuwakinga watumishi dhidi ya maambukizi na kuhakikisha usalama wao, tumepunguza idadi ya watumishi katika kila zamu, pamoja na kuwapuliza dawa kila wanapo maliza kufanya kazi”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua hatua mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na imefanyia kazi maelekezo yote yanayo tolewa na sekta ya afya, katika kiwango cha Ataba tukufu, mji mkongwe na mkoa kwa ujumla, kitengo kinacho simamia eneo la katikati ya haram mbili takatifu kina mchango mkubwa katika utekelezaji wa shughuli hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: