Jana usiku watumishi wa kitengo cha kusimamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu pamoja na wale wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamemaliza kutandika busati jekundu katika uwanja wa katikati wa haram mbili, uwanja huo unakadiriwa kuwa na ukubwa wa zaidi ya mita (14000), ikiwa ni sehemu ya kujiandaa kupokea waombolezaji wa siku ya Ashura (mwezi kumi Muharam), busati hilo litarahisisha utembeaji wao.
Haya yamesemwa na rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi: “Busati hili pia limetandikwa kuanzia mlango wa Atabatu Husseiniyya takatifu kwa kupitia kwenye uwanja uliotajwa hadi kwenye milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu mkabala wake, nayo ni: (Mlango wa Imamu Hassan, na mlango wa Imamu Hussein na mlango wa Imamu wa zama –a.s-)”.
Akafafanua kuwa: “Pamoja na kutandikwa busati jekundu, tumetandika pia nailoni chini ya busati ili kuwafanya mazuwaru watembee vizuri, ukizingatia kuwa chini kuna marumaru ambazo hutatiza kidogo kutembea juu yake”.
Kumbuka kuwa kitengo hiki ni sawa na vitengo vingine vya Ataba mbili takatifu, kinafanya kila kiwezalo kuboresha mazingira ya mazuwaru na mawakibu Husseiniyya, sambamba na kutekeleza maagizo yote ya kujikinga na maambukizi, yaliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu pamoja na sekta za afya zenye dhamana.