Waziri wa Afya wa Iraq Dokta Hassan Tamimi amesema kuwa huduma za afya na mfumo wa kijikinga na maambukizi unaofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, katika kipindi hiki ambacho imejiandaa kupokea mazuwaru wanao omboleza Ashura mwaka huu 1442h una umakini mkubwa, unasaidia sana kuzuwia maambukizi na kudhibiti idadi ya wagonjwa bila kutokea visa vya ziyada.
Ameyasema hayo alipo tembelea Atabatu Abbasiyya tukufu Alasiri ya leo siku ya Ijumaa mwezi (8 Muharam 1442h) sawa na tarehe (28 Agosti 2020m) na kuangalia hatua za kujikinga na maambukizi zinazo fanywa na Ataba katika kipindi hiki cha Ziyara ya Ashura, aliongozana na mkuu wa idara ya afya ya mkoa wa Karbala, na wakapokewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu.
Akaongeza kuwa: “Tunatoa shukrani na pongezi kubwa kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa namna inavyo pambana na janga la Korona, pamoja na jinsi inavyo isaidia wizara ya afya na madaktari katika kupambana na janga hili, wala sio katika mkoa wa Karbala peke yake bali kwenye mikoa yote ya Iraq”.
Kumbuka kuwa Itabatu Abbasiyya tukufu tangu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam imekuwa ikizingatia kanuzi za afya katika kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na kufanyia kazi maelekezo yote yaliyo tolewa na sekta husika.