Rais wa umoja wa viongozi wa kusimamia mali ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Adhururi ya Ijumaa ya leo mwezi (8 Muharam 1442h) sawa na tarehe (28 Agosti 2020m), rais wa viongozi wa kusimamia mali Dokta Raafil Yaasin ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, na kupokelewa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Ustadh Jawadi Hasanawi.

Wamejadili baadhi ya miradi inayofanywa na Atabatu Abbasiyya kwenye sekta tofauti, ambayo inatoa huduma kwa wananchi, hususan miradi ambayo imeanza kutekelezwa katika mazingira ya maambukizi ya virusi vya Korona.

Mwisho wa kikao chao, Dokta Raafil akapongeza kazi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kila sekta, kisha akaagwa kwa bashasha kama alivyo pokewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: