Vituo vya Ashura: Mwezi tisa Muharam iliwasiri barua ya ibun Ziyadi iliyo amrisha kuuwawa Imamu Hussein (a.s) na kuzingira mahema yake

Maoni katika picha
Kitabu cha Arbaabu Maqaatil kimeandika kuwa katika siku kama ya leo mwezi tisa Muharam mwaka 61h, Mal-uni Shimri alipeleka barua ya Ubaidullahi bun Ziyadi kwa Omari bun Saadi, isemayo: Mimi sijakutuma kwa Hussein ukamlinde, kukaa nae, kumpa amani, kumuombea msamaha, wala kuwa msemaji wake kwangu, tambua kama Hussein na watu wake wakikubali kutii utawala wangu, wajisalimishe na uwalete kwangu kwa amani na kama wakikataa, watese hadi uwauwe na udhalilishe maiti zao, hakika wanastahiki kufanyiwa hivyo, ukimuuwa Hussein amrisha farasi zikanyage kanyage kifua chake..

Omari bun Saadi alipo isoma akasema: una nini? Mwenyezi Mungu hatakuwa karibu na nyumba yako, hapendi jambo uliloniletea, wallahi Hussein hawezi kujisalimisha, hakika yeye ni mtu mwema, Shimri akasema: niambie utafanya nini? Tekeleza amri ya kiongozi wako, kama hauwezi niachie mimi niongoze jeshi, akasema: hapana.. mimi nasimamia jambo hilo, wewe ongoza wapiganaji wa miguu..

Katika siku hiyo wakazingira mahema ya Imamu Hussein (a.s), imepokewa kutoka kwa Abu Abdillahi Swadiq (a.s) anasema: (Mwezi tisa ndio siku aliyo zingirwa Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake (r.a) katika ardhi ya Karbala, watu wa Sham walikusanyika kumzingira na akafurahi ibun Marjana na Omari bun Saadi kutokana na wingi wao, walifurahia udhaifu wa jeshi la Hussein (a.s) na wafuasi wake, wakaamini kuwa hakuna yeyote atakaekuja kumsaidia Imamu Hussein (a.s), hivyo ni dhaifu na mgeni).

Kisha akasema: (Siku ya mwezi kumi (Ashura) ndio siku aliyo uwawa Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake (r.a), hivi swaumu ndio inakuwa katika siku hiyo?!! Hapana sio siku ya kufunga bali ni siku ya huzuni na msiba mkubwa kwa viumbe wa mbinguni na aridhini pamoja na waumini wote, aidha ni siku ya furaha kwa ibun Marjana na Aali Ziyadi na watu wa Sham –Mwenyezi Mungu amewakasirikia pamoja na familia zao- aridhi yoto ilimlilia siku hiyo ispokua aridhi ya Sham, atakaefunga siku hiyo au akasherehekea Mwenyezi Mungu atamfufua pamoja na Aali Ziyadi akiwa amewakasirikia, atakae ingiza zawadi katika nyumba yake siku hiyo Mwenyezi Mungu ataingiza unafiki katika moyo wake hadi siku atakayo kutana nae, na atamuondolea baraka pamoja na familia yake na watoto wake na atakuwa mshirika wa shetani katika kila kitu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: