Bendera (58) za kuomboleza msiba wa Imamu Hussein zinapepea kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu

Maoni katika picha
Hali ya malalo mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) imejaa huzuni na majonzi, hivyo hivyo katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, ukiwa ni muendelezo wa mazingira sawa na hayo yaliyopo ndani ya Ataba mbili tukufu na sehemu zinazo zunguka Ataba bizo.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili Sayyid Naafii Mussawi, amesema kuwa: “Miongoni mwa ishara za huzuni katika uwanja wa katikati ya haram mbili ni kuwepo kwa bendera (58) zinazo ashiria umri wa Imamu Hussein (a.s), zimewekwa kwenye nguzo za taa zilizopo pembezoni mwa uwanja huo, na zimeandikwa: (Amani iwe juu yako ewe bwana wa mashahidi) na zingine zimeandikwa (Ewe mwezi wa bani Hashim) kwa rangi nyekundu, aidha uwanja huo umewashwa taa nyekundu, hali kadhalika yamewekwa mapambo meusi kwenye uzio unao zunguka eneo hilo takatifu, kuashiria huzuni na majonzi yaliyotanda katika Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: