Kufanya ziara maalum ya Ashura kwa niaba

Maoni katika picha
Idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuwa siku ya kesho mwezi kumi Muharam, watafanya ziara maalum –Ashura- ya Imamu Hussein (a.s) pamoja na ziyara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuswali rakaa mbili na kusoma dua kwa niaba ya watu waliojisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba uliopo kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo Sayyid Hashim Shami, amesema: “Kwa baraka za tunae muomboleza leo tumemaliza sehemu ya kwanza ya kufanya ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa niyaba, ziara hizo zimefanywa na kundi la Masayyid ambao ni watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wamekuwa wakifanya ziara hizo kila siku tangu siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam hadi siku ya tisa, na sasa hivi tunajiandaa kufanya ziara maalum itakayo kamilisha ziara zote tulizo fanya siku za nyuma”.

Akasisitiza kuwa: “Tunaona fahari kutoa huduma hii na tunatoa wito kwa kila aliyeshindwa kuja katika ardhi hii takatifu kumpa pole Imamu wa zama (a.f) kwa kuuwawa babu yake Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake (r.a) ajisajili kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/ na sisi tutamfanyia ziara na kumuombea dua mbele ya malalo mawili matakatifu, yeye na wanao muhusu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: