Ibada za usiku wa mwezi kumi Muharam

Maoni katika picha
Usiku wa mwezi kumi Muharam, ni usiku mtukufu ambao Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake walikesha wanaswali na kuomba dua, walitaka kukutana na Mwenyezi Mungu mtukufu wakiwa na nyoyo salama na nafsi tulivu, waliomba msamaha na rehema kwa Mwenyezi Mungu, walikesha wanafanya ibada na kuswali, hakuna aliyelala katika usiku huo kama inavyo ripotiwa na vitabu vya historia.

Miongoni mwa ibada za usiku huu ni:

Kuswali rakaa mia moja, kila rakaa unasoma Alhamdu na (Qul-huwallahu Ahadun) mara tatu, baada ya kumaliza kuswali rakaa zote utasema: Subhana Llahi wal-hamdulilaahi wa laa ilaaha illaa Llahu wa Llahu Akbaru, walaa haula walaa quwata ilaa billahi Al-Aliyyi Al-Adhim (mara sabini), imepokewa kuwa unaweza kusoma istighfaar pia baada ya neno (Al-Aliyyi Al-Adhim).

Katika riwaya nyingine utaswali rakaa nne mwishoni mwa usiku, katika kila rakaa baada ya Alhamfu utasoma ayatu Kursiyyu, Tauhiid, Falaq na Naasi (mara kumi), kisha unasoma surat Tauhiid baada ya salam mara mia moja.

Kuswali rakaa nne, kila rakaa unasoma Alhamdu na surat Tauhiid mara hamsini, swala hii ni sawa na swala ya kiongozi wa waumini (a.s) kwa utukufu.

Baada ya swala hiyo mtaje Mwenyezi Mungu kwa wingi na umswalie Mtume pamoja na kuwalaani maadui zao kwa kiasi utakavyo weza.

Imepokewa kuwa atakaefanya ibada katika usiku huu ataandikiwa thawabu za ibada za malaika wote, na thawabu za ibada ya miaka sabini, na atakae mzuru Imamu Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala na akalala hapo hadi asubuhi, atafufuliwa siku ya kiyama akiwa amelowana damu ya Hussein (a.s) pamoja na mashahidi waliokufa na Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: