Kamanda makini alikataa kupewa amani

Maoni katika picha
Msimamo wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika vita ya Twafu, ni msimamo wa pekee katika historia ya kiislamu na kibinaadamu, alisimama imara bila kutetereka katika kumlinda ndugu yake bwana wa mashahidi (a.s), alikataa amani aliyopewa na Shimri bun Dhijausheni (laana iwe juu yake) kwa hoja ya ujomba aliyonayo na mwezi wa bani Hashim (a.s), kalamu haziwezi kuandika sifa zake na ndimi haziwezi kutaja mema yake zikamaliza.

Imepokewa kuwa Shimri (laana iwe juu yake) alikuja nakasema: Wako wapi watoto wa dada yetu? Akimkusudia Abbasi na wadogo zake, wadogo zake Abbasi wakakaa kimywa kutokana na kumuheshimu kaka yao, na Abbasi akakaa kimywa kutokana na kumuheshimu Imamu Hussein (a.s), Shimri akaita tena, Abulfadhil Abbasi akaendelea kukaa kimywa bila kumjibu, Hussein (a.s) akasema: (Mjibu japokuwa ni muovu).

Akasema (kumuambia Shimri): Una nini? Na unataka nini?

Enyi watoto wa dada yangu nakupeni amani, msikubali kufa pamoja na Hussein, mtiini kiongozi wa waumini Yazidi.

Abbasi akasema: Mwenyezi Mungu akulaani na alaani amani yako!! Unatupa amani wakati mtoto wa Mtume hana amani, unatutaka tumtii aliye laaniwa na watoto wa walio laaniwa?

Hapa unaonekana utukufu wa Abbasi (a.s) alichagua kufa katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kumnusuru (a.s) na sio kukubali kuwa chini ya viongozi madhalimu, hakukubali kutengana na ndugu yake kwa namna yeyote ile, alibakia na msimamo huo hadi dakika ya mwisho ya uhai wake, akauwawa kishahidi pembeni ya mto Furaat, baada ya kupigana vita kali, kama anavyo sema mshairi:

Alisonga mbele kwa haraka kwenye vita ** kana kwamba anakwenda kwenye amani.

Hakika msimamo wa Abulfadhil Abbasi (a.s) unaendelea kuwa shule ya milele isiyo isha, vizazi na vizazi vinajifunza kutokana na ushujaa wake namna ya kulinda misingi ya utukufu, ardhi na maeneo matakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: