Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake walihuisha vipi usiku wa mwezi kumi Muharam

Maoni katika picha
Watu wa historia wanasema kuwa Imamu Hussein (a.s) alimuambia ndugu yake Abbasi (a.s) Alasiri ya mwezi tisa Muharam mwaka 61h, aliombe jeshi la Umawiyya waahirishe vita katika usiku wa mwezi kumi hadi mchana wake ili wautumie usiku huo kwa kufanya ibada, kuswali, kusoma dua na kufanya maghfira.

Taarikh Twabari imeandika kuwa: Hussein (a.s) alimuambia ndugu yake Abbasi: “Rudi kwao ukawaombe waahirishe vita hadi kesho, ili tuweze kutumia usiku huu kuswali na kusoma dua, hakika anatambua mimi napenda kuswali na kusoma Quráni pamoja na kusoma dua kwa wingi na kufanya istighfaar”.

Imamu Hussein na watu wake walihuisha vipi usiku wa mwezi kumi Muharam?

Ibun Kathiir amepokea kutoka kwa Haarith bun Kaabi na Abu Dhwahaak, kutoka kwa Ali bun Hussein -Zainul-Aabidina- (a.s) anasema: Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake walikesha usiku mzima wanaswali na kufanya maghfira, huku wamezungukwa na farasi za maadui wao, Imamu Hussein (a.s) alikuwa akisoma kwa wingi aya zisemazo: (Wala wasidhani wale wanao kufuru kwamba huu muhula tunao wapa ni kheri kwao. Hakika tunawapa muhula wazidi madhambi. Na yao wao ni adhabu ya kuwadhalilisha * Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwaacha waumini katika hali mliyo nayo mpaka apambanue wabaya na wema).

Hivi ndio wanahistoria na wapokezi wa hadithi wengine walivyo ripoti, kuwa Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake walihuisha usiku wa Ashura kwa kufanya ibada, waliswali, kusoma dua na kuomba maghfira.

Mpokezi mmoja anasema: (Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake katika usiku huo walikuwa wanasikika kama sauti za kundi ya nyuki, kila mtu alikuwa ima kasujudu au karukuu au kasimama au kakaa, Imamu Hussein (a.s) alikuwa anapenda sana kuswali).

Katika kitabu cha Ansaabu Ashraafu imeandikwa kuwa: (Ulipo ingia usiku, Hussein (a.s) na wafusi wake waliswali usiku mzima na kufanya tasbihi na kuomba dua na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: