Matukio ya mwezi kumi Muharam asubuhi

Maoni katika picha
Imamu Hussein (a.s) na watu wake walianza siku yao kwa swala ya Asubuhi ya jamaa, kisha (a.s) akapanga safu za wapiganaji wake, wapanda farasi walikua thelathini na mbili na watembea kwa miguu arubaini.

Zuhairu bun Qayin akamuweka upande wa kulia, na Habibu mun Mudhwahir upande wa kushoto, bendera akamkabidhi ndugu yake Abbasi bun Ali (a.s), akawaambia wafuasi wake waweke hema zao karibu karibu na wengine wakae ndani ya mahema, wajikusanye wote sehemu moja ili wakabiliane na adui kutokea upande mmoja, akaamuru wakusanye kuni na kuzipanga nyuma yao kwenye shimo (mtaro) waliokuwa wamechimba usiku, lilikuwa kama handaki, wakaweka humo majani na kuni, akasema: “wakitaka kutushambulia kwa nyumba washeni moto ili wasiweze kutupiga kwa nyuma”.

Upande wa pili Omari bun Saadi alikusanya jeshi lake, lililokuwa na askari elfu nne, Omari bun Saadi akamuweka upande wake wa kulia Amru bun Hajjaaji Azubaidiy, na kushito Shimri bun Dhijaushen Dhwabaabi, na kikosi cha farasi kikaongozwa na Azrah bun Qaisi Ahmasiy, na kikosi cha miguu Shabthu bun Rabii Riyahi.

Omari bun Saadi upande wa watu wa Madina akamuweka Abdullahi bun Zuhair Azadiy, na upande mwingine akamuweka Rabia na Kindah Qaisi bun Asháth bun Qais, na upange mwingine Abdurahmaani bun Abi Sabra Jaáfiy, na Tamimi na Hamdani Alhurru bun Yadidi Riyahi, na akampa bendera Daridan na wakajiandaa kupigana na Abu Abdillahi Hussein (a.s) na wafuasi wake.

Riwaya zinasema kuwa, Imamu Hussein (a.s) alipoangalia jeshi la maadui aliinua mikono juu na akasema: “Ewe Mola wewe ndio kimbilio langu katika kila kitu, nakutegemea katika kila shida, wewe ni wangu katika kila jambo linalo nisibu, matatizo mangapi yanayo vunja moyo na kupunguza nguvu, yanamuumiza rafiki na kumfurahisha adui, niliyo yashitakia kwako, nikiwa na matumaini makubwa kwako wala sio kwa mwingine zaidi yako, ukanifariji na kuniondolea, wewe ndio mkuu wa kila neema, na mwenye kila jema na kilele cha kila tarajio”.

Omari bun Saadi akatuma watu kwenda kushambulia mahema upande wa kulia na kushoto kwao, Akasema: wakaondoka watu watatu au wanne upande wa Imamu Hussein (a.s) wakawa wanapambana na kila anayetaka kushambulia hema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: