Muhimu kwa picha… kuanza matembezi ya (Towareji)

Maoni katika picha
Baada ya swala ya Adhuhuri mwezi kumi Muharam (1442h) sawa na (30 Agosti 2020m) yalianza matembezi ya Towareji, yameanzia katika kituo cha Salaam kupitia barabara ya Jamhuriyya hadi kwenye Atabatu Husseiniyya tukufu kisha katika uwanja wa katikati ya haram mbili hadi kwenye Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ulinzi na usalama uliimarishwa maeneo yote yaliyo tanjwa sambamba na huduma za afya, watumishi wa Ataba mbili tukufu wamejizatiti kuhakikisha matembezi hayo yanafanyika kwa utulivu na amani.

Matembezi ya Towareji hufanywa na watu wengi, yalianza kufanywa na watu wa kabila la Towareji, (Towareji ni wilaya iliyopo katika mkoa wa Karbala umbali wa km 20), kama sehemu ya kuitikia wito wa Imamu Hussein (a.s) siku ya mwezi kumi Muharam, pale aliposema (Je kuja wakuninusuru aje kuninusuru), moja ya vituo vya takwimu vilisema kuwa matembezi hayo ndio mkusanyiko mkubwa zaidi wa watu duniani na wapekee. Yalianza mwaka (1303h) sawa na mwaka (1885m).

Wazee wanahadithia kuwa mwezi kumi Muharam baada ya kumaliza kusoma maqtal katika nyumba ya Sayyid Swalehe Kazwini lilitoka kundi la watu wakisema (Waa Hussein.. waa Hussein) kisha yakaratibiwa vizuri matembezi katika miaka iliyofuata, wakawa wanatembea hadi Karbala mwezi kumi Muharam baada ya swala ya Adhuhuri, sehemu yanapo anzia matembezi hayo inaumbali wa (km5) hadi kufika kwenye kaburi la Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: