Vituo vya Ashura: Safari ya mateka wa Imamu Hussein (a.s) kutoka Karbala hadi Kufa baada ya mauwaji

Maoni katika picha
Mwezi kumi na moja Muharam mwaka 61h, watu wa nyumba ya Mtume (a.s) waliotekwa kwenye msafara wa Imamu Hussein (a.s) walitolewa Karbala na kupelekwa katika mji wa Kufa.

Omari bun Saadi alibaki Karbala hadi Adhuhuri akaswalia watu waliokufa katika jeshi lake na kuwazika, ulipo fika mchana akawabeba watu wa Imamu Hussein (a.s) ambao ni wanawake watakatifu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) juu ya ngamia wasiokuwa na tandiko za kukalia wala kijumba, kisha wakaanza safari ya kwenda Kufa, wakati wanaondoka wakaangalia mwili wa bwana wa mashahidi Hussein (a.s) ukiwa umelala juu ya udongo umezungukwa na miili ya mashahidi iliyosambaa kwenye ardhi ya Karbala!.

Wakati huo ibun Saadi alikuwa amesha kata vichwa vya miili hiyo na kuvituma Kufa, msafara huo ulikuwa wa mateka ambao ni wanawake na watoto wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) pamoja na baadhi ya watoto wa wafuasi wake.

Bibi Zainabu mtoto wa kiongozi wa waumini (a.s) alisimama karibu na mwili wa kaka yake Hussein (a.s) akasema: (Waa Muhammadaahu! Alikutakia rehma mfalme wa mbingu, huyu Hussein kwenye mavumbi, amelowa damu, amekatwa katwa viungo, na mabinti zako tumetekwa, na familia yako imeuwawa!!).

Kisha jabali wa subira.. akalia sana kwa uchungu mkubwa, miezi mitakatifu imeuwawa kikatili na miili yao kusulubiwa na wanawake wametekwa.

Aliondoka akiwa na uchungu mkubwa sana, nyuma yake miili na mbele yake vichwa vya mashahidi, huku mayatima na wajane wakiwa wamemzunguka, amekaa juu ya ngamia asiekuwa na tandiko, naye ni binti wa yule ambaye daraja lake kwa Mtume ni sawa na Haruna kwa Mussa na mama yake ni mbora wa wanawake wa ulimwenguni..

Hapo ikaanza hatua nyingine katika hatua za Ashura, bibi Zainabu (a.s) akawa mhimili muhimu katika hatua hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: