Kwa picha: Kuhuisha usiku wa mwezi kumi na moja Muharam (usiku wa upweke)

Maoni katika picha
Wakazi wa mji mtukufu wa Karbala wameendeleza utamaduni wao wa kuomboleza usiku wa mwezi kumi na moja Muharam kila mwaka (usiku wa upweke) kwa Imamu Hussein (a.s), jioni ya Jumapili mwezi (10 Muharam 1442h) sawa na tarehe (30 Agosti 2020m) kundi kubwa la mazuwaru limekwenda kuzunguka malalo ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Wamekesha wanaomboleza wakiwa na nyoyo za huzuni na nyuso zilizojaa vumbi la udongo wa Karbala, kumpa pole bibi wa subira Zainabu Alkubra (a.s) kwa kuuwawa ndugu zake na kuchomwa hema zao, wamesoma mashairi na matam. Waombolezaji wamewasha mishumaa katika eneo la katikati ya haram mbili na jirani na Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya, macho yao yamebubujika machozi kwa uchungu kutokana na yaliyo jiri kwa familia ya Mtume (s.a.w.w), na mateso aliyopitia bibi Zainabu (a.s) pamoja na watoto wa familia ya Imamu Hussein (a.s) baada ya kifo chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: