Kumaliza kazi ya kusafisha haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya kusimamia haram tukufu na walioshirikiana pamoja nao kutoka vitengo vingine vya Ataba tukufu, wamemaliza kufanya usafi kwenye haram tukufu, wametoa vitu vyote vilivyo wekwa kwa ajili ya kupokea mawakibu za waombolezaji na mazuwaru wa ziara ya mwezi kumi Muharam.

Wametumia wakati wa usiku kufanya kazi hiyo, kutokana na uchache wa mazuwaru wakati huo, wametandua busati lekundu pamoja na viambata vyake, sambamba na kutoa mchanga kwenye sehemu za milango halafu wakafagia na kupiga deki sehemu yote ya haram takatifu na kuirudisha katika mazingira yaliyokuwepo kabla ya kipindi cha ziara.

Kumbuka kuwa vitengo vya Atabatu Abbasiyya baada ya kutangaza kufanikiwa katika mkakati wa ziara ya mwezi kumi Muharam, vimeingia katika hatua ya pili ya kufanya usafi ndani na nje ya Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: