Alasiri ya Jumatano mwezi (13 Muharam 1442h) sawa na tarehe (2 Septemba 2020m) yamehitimishwa maombolezo ya kabila la bani Asadi pamoja na makabila mengine ya Iraq, waliyofanya kukumbuka mazishi ya miili ya mashahidi wa Twafu (a.s).
Atabatu Abbasiyya tukufu imetumia uwezo wake waote kuhakikisha shughuli hiyo inakamilika kwa utulivu na amani kama ilivyo kawada ya mwezi (13) Muharam kila mwaka, aidha imetangaza kufanikiwa kwa mkakati wake wa ulinzi na utumishi ndani ya siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam.
Mafanikio haya yamepatikana kutokana na kushirikiana pamoja na Atabatu Husseiniyya tukufu na vyombo vya ulinzi na usalama bila kusahau idara ya afya ya mkoa huu, na watu waliokuja kujitolea kufanya kazi pamoja na ndugu zao watumishi wa Ataba tukufu, mafanikio haya ni sehemu ya muendelezo wa mafanikio yaliyo tangulia katika uratibu wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu.
Kumbuka kuwa mji mtukufu wa Karbala baada ya Adhuhuri ya leo umeshuhudia maukibu ya kabila la bani Asadi pamoja na makabila mengine ya Iraq, wakikumbuka mazishi ya miili mitakatifu ya mashahidi wa Twafu.
Tambua kuwa tukio hili hufanywa kila mwaka, makabila ya Karbala na maeneo yanayo izunguka yamezowea kufanya hivyo, tukio hili limekuwa kielelezo cha uwepo wa Irag.