Bango kubwa zaidi la uombolezaji katika mji wa Karbala limefunika sura ya kituo cha matangazo na masoko Alkafeel

Maoni katika picha
Sura ya kituo cha matangazo na masoko Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya imefunikwa na bango kubwa zaidi ya uombolezaji katika mkoa wa Karbala, bango hilo limesanifiwa na kutengenezwa na kitengo maalum cha kuomboleza msiba wa kukumbuka kifo cha mjukuu wa Mtume Imamu Hussein (a.s), kufuatia maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliyehimiza kuweka mazingira ya huzuni, bango hili ni alama ya wazi na limefunika sura ya kituo, linaukubwa wa mita 144.

Akaongeza kuwa: “Bango hilo limeandikwa maneno yasemayo (Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako ewe Imamu wa zama) kwa kuwa yeye ndio mfiwa mkuu katika msiba huu, yakifuatiwa na picha ya kubba na minara ya kamanda wa jeshi la Imamu Hussein (a.s) na mbeba bendera wake Abulfadhil Abbasi (a.s) na sehemu ya dirisha takatifu pamoja na ngao na mkuki uliolowa damu, kwa ndani linaonekana neno lisemalo (Ewe Abulfadhil Abbasi)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: