Vituo vya Ashura: Imamu Zainul-Aabidina (a.s) amuambia ibun Ziyadi.. Unanitishia kifo! Hautambui kuwa kuuwawa ni kawaida kwetu na utukufu wetu mbele ya Mwenyezi Mungu ni shahada

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa katika siku kama hizi mwaka 61h, Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alisimama kwa ushujaa mbele ya Ubaidullahi bun Ziyadi, akiwa ni mateka aliyefungwa minyororo, huku ibun Ziyadi anachomachoma mdomo wa baba yake kwa fimbo, huzuni aliyokua nayo haikumzuwia kuongoe kwa ushujaa mbele yake pamoja na kutishiwa kuuwawa.

Matashi ya Mwenyezi Mungu yalikuwa tofauti na alivyotaka ibun Ziyadi, mjadala baina yao uliishia kwa ibun Ziyadi kuamrisha akatwe shingo Imamu (a.s), shangazi yake Hauraa Zainabu akamkumbatia mtoto wa kaka yake na akasema kumuambia ibun Ziyadi: (Haujabakisha yeyote katika sisi kama umekusudia kumuua basi niuwe pamoja nae), Imamu Sajjaad (a.s) hakurudi nyuma wala hakuogopa, alizungumza maneno makali yanayo onyesha kuwa haogopi kuuwawa, alimuambia kwa kujiamini kuwa: (Unanitishia kifo!! Hautambui kuwa kuuwawa ni kawaida kwetu na utukufu wetu mbele ya Mwenyezi Mungu ni shahada).

Hakika ushujaa alio onyesha Imamu Sajjaad (a.s) baada ya tukio la Karbala, akiwa mgonjwa na mateka ni sawa na wale walioingia katika uwanja wa vita, hapo sio sehemu pekee aliyo onyesha msimamo mbele ya madhalimu baada ya kuuwawa baba yake na watu wa nyumbani kwake (a.s), alionyesha msimamo katika mji wa Kufa kupitia khutuba yake tukufu aliyo eleza dhambi kubwa iliyofanywa na bani Umayya, kwa kumuuwa mjukuu wa Mtume na watu wa kufa kuwageuka, maneno ambayo yaliamsha chuki na hasira dhidi ya Yazidi, alisema (a.s): (Enyi watu! Aliyekuwa ananijua basi ananijua, na asiyenijua mimi ni Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s). mimi ni mtoto wa aliyechinjwa pembezoni mwa mto wa Furaat bila kosa.

Mimi ni mtoto wa aliyevunjiwa heshima yake, akaporwa neema yake na mali zake, na imetekwa familia yake. Mimi ni mtoto wa aliyeuwawa akiwa na subira na hilo latosha kuwa fahari. Enyi watu! Nakuambieni kwa haki ya Allah! Mnatambua kuwa mlimuandikia baba barua kisha mmemhadaa? Mkamuahidi na kula kiapo cha utii (baiyya) kwake, kisha mmemtenga na kumuuwa? Mmeangamia kwa mliyo fanya kwa nafsi zenu, mtamuangalia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kwa jicho gani? Atakapo kuambieni: Mliuwa kizazi changu, na mkavunja heshima yangu, nyie sio katika umma wangu?). maneno hayo yalikuwa makali na yanachoma, yaliamsha hasira na chuki kwa watawala, sauti za watu zikasikika kutoka kila upande wakiambiana: Mmeangamia kwa mliyo fanya. Pamoja na majonzi aliyokuwa nayo Imamu (a.s) aliongea kwa ujasiri akawaambia: Mwenyezi Mungu amrehemu atakaekubali nasaha zangu, na akahifadhi usia wangu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na watu wa nyumbani kwake, hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kiigizo chema kwetu.

Wakasema wote kwa pamoja: Sisi wote –ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu- Tumekusikia, tunatii, tutahifadhi dhima yako, hatutakupuuza wala kukuasi tuambie utakacho Allah akurehemu, hakika tutapigana pamoja na wewe na tutakuwa pamoja na wewe, tutalipa kisasi kwa Yazidi! Na tunajitenga na waliokudhulumu na wakatudhulumu!

Akasema (a.s): Iwe mbali! Iwe mbali: Enyi watu wa hila na vitimbi, kuna pazia kati yenu na matamanio ya nafsi zenu! Mnataka kuniletea mliyo waletea baba zangu kabla?! Hapana na ngonjera zenu, hakika kidonda bado hakijapona, jana kauwawa baba yangu –a.s- pamoja na watu wa nyumbani kwake, bado sijasahau uzito wa msiba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na wa baba yangu na watoto wa baba yangu, na mwili wake ukiwa umetelekezwa, na uchungu wake bado upo kooni kwangu, na majonzi yake yamejaa kifuani mwangu, na mambo yangu yasiwe kwetu wala juu yetu).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: