Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake imefungua mlango wa usajili wa kushiriki katika semina zake za Quráni

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, imetangaza kufungua milango ya usajili wa semina zake mbalimbali kuhusu Quráni tukufu zitakazo endeshwa kwa njia ya mtandao kupitia majukwaa maalum, chini ya ukufunzi wa wabobezi wa masomo ya Quráni pamoja na kuangalia umri wa kila kundi.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa Maahadi bibi Mannaar Jawaad Jaburi amesema: “Katika kuendeleza mwenendo wa Maahadi ya Quráni na malengo matukufu ya kuanzishwa kwake, kama kawaida Maahadi imeratibu semina zitakazo tolewa na kituo cha Najafu au kupitia matawi yake yaliyopo mikoani, semina hizo zitaendeshwa kwa njia ya mtandao, kutokana na mazingira ya sasa ambayo hayaruhusu mikusanyiko kufuatia uwepo wa maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akaendelea kusema: Usajili unaofanywa ni wa semina za (Usomaji – kuhifadhi – hukumu za tajwidi – kujifunza usomaji sahihi), pamoja na vipengele vingine, usajili unafanywa kwa njia ya mtandao, kupitia link ifuatayo: shorturl.at/hRSX6.

Kumbuka kuwa semina hizi hupewa kipaombele sana na Maahadi, miongoni mwa harakati zake semina zina umuhimu mkubwa, uongozi wa Maahadi huzipa nafasi maalum kutokana na faida inayo patikana, ya kutengeneza kizazi cha wasomi wazuri wa kike, kutokana na mazingira ya sasa pamoja na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na idara ya afya kuzuwia mikusanyiko, sambamba na marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, Maahadi imelazimika kutumia njia hii kuendelea kusomesha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: