Chuo kikuu Alkafeel kinaendesha program ya kugawa maji safi ya kunywa kwenye vituo vya mitihani ya wanafunzi wanahitimu masomo yao

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanzisha program kwa jina la (Alkafeel) ya kuwasaidia wanafunzi wanao fanya mitihani ya kuhitimu masomo, kwa kuwapa maji ya kunywa (chupa za maji) pamoja na barakoa, chini ya utaratibu unaowezesha kufikia vituo vyote vya mitihani hapa mkowani.

Kwa mujibu wa maelezo ya Dokta Nawali Aaidi Almayali makamo rais wa chuo, amesema: “Opreshesheni hii inaendana na utaratibu wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kipindi hiki cha maambukizi ya virusi vya Karona, aidha ni sehemu ya kutekeleza wajibu wake kibinaadamu na kitaifa sambamba na kufanyia kazi maelekezo ya rais wa chuo Dokra Nuris Dahani, ya kusaidia wanafunzi wakati wa mitihani ya wizara hususan mwaka huu ambao wanafunzi wapo katika mazingira ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Akaongeza kuwa: “Opresheni inasimamiwa na kundi la watumishi wa chuo kwa kushirikiana na idara ya mkoa wa Najafu, tunagawa chupa za maji safi ya kunywa pamoja na barakuo na vitakasa mikono”.

Wasimamizi wa idara ya malezi, walimu na wanafunzi kwa ujumla wameshukuru sana na kusifu hii program, ambayo ni muhimu sana kwa wanafunzi, ni wazi kuwa watanufaika sana na msaada huo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: