Vituo vya Ashura: Mfuasi wa Haidari amkemea ibun Ziyadi na wenzake

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa, askari wa ibun Ziyadi walipoingia katika Qasri la utawala, waliweka kichwa cha Imamu Hussein (a.s) mbele yake, akaanza kuchomachoma meno matakatifu ya Imamu (a.s) kwa fimbo aliyokuwa nayo mkononi, Zaidu bun Arqam akamuambia: Ondoa fimbo yako kwenye mdomo huo mtakatifu; Naapa kwa yule ambae hakuna Mungu ispokuwa yeye niliona mdomo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ikibusu mdomo huo, kisha akalia. Ibun Ziyadi akasema: Mwenyezi Mungu ayalize macho wako, wallahi kama usingekuwa mzee uliyechoka na kupungukiwa akili yako ningekata shingo lako.

Zaidu akatoka huku akisema: Enyi waarabu mmekuwa watumwa baada ya leo, mmeuwa mtoto wa Fatuma na mmemtawalisha ibun Marjana, anauwa watu wema miongoni mwenu na kuwatukuza waovu wenu, mmeridhia udhalili, niwe mbali na watu wanaokubali udhalili, ibun Ziyadi alipo baini kuwa watu wameanza kubadilika, hususan baada ya kuongea bibi Zainabu, aliogopa hasira za watu, akaamrisha askari wawapeleke mateka kwenye nyumba iliyokuwa karibu na msikiti mkubwa, Hajibu bun Ziyadi anasema kuwa: Nilikuwa pamoja nao wakati alipo amrisha wapelekwe jela, nikawaona wanaume na wanawake wanalia na kupiga nyuso zao.

Bibi Zainabu akasema: Asiingize yeyote kwetu ispokua mtumwa au mama wa mtoto, hakika wao wametekwa kama tulivyo tekwa.

Akimaanisha kuwa aliyetekwa anajua uchungu wa udhalili, jambo hilo liko wazi halipingiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: