Kituo cha utamaduni wa familia kimeanza program ya (kitabu changu thamani yangu) awamu ya nne

Maoni katika picha
Katika kuendeleza awamu tatu zilizo tangulia kwa mafanikio, kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza awamu ya nne ya program ya (kitabu changu thamani yangu), inayo lenga wasichana wa umri tofauti.

Program hii inalenga kuinua kiwango cha maarifa kwa mwanamke na kutumia vizuri muda kwa faida yake, kutokana na wingi wa maombi ya ushiriki program imeendelea hadi kufikia awamu hii.

Haya yamesemwa na mkuu wa kituo Ustadhat Asmahani Ibrahim, akaongeza kuwa: “Mkono utakao nyooshwa maktaba kufanya utafiti unamaanisha akili, fikra na uwepo, tusome kitabu kwa hekima na mawaidha ili tuwashe nuru ya fikra na kuondoa giza la ujinga, kwa ajili hiyo tumeanza awamu ya nne ya program ya (kitabu changu thamani yangu) ambayo kituo cha utamaduni wa familia kinaichukulia kama mnara wa wanawake na waumini, wanaulizwa maswali yanayo lenga kupima uwelewa wao na jinsi wanavyo weza kuutumia katika maisha ya kila siku, zimetengwa siku 15/ kumi na tano za kujisomea na kujibu maswali, pamoja na kuandaa zawadi za washindi watatu watakao patikana baada ya kupigiwa kura”.

Akaongeza kuwa: “Program itaendeshwa kwa njia ya mtandao na ushiriki utafanyika kupitia link ifuatayo: https://forms.gle/5Tr9EWqb8NL2D9Fm8

Kumbuka kuwa program inalenga kuamsha roho zilizo lala katika maswala ya usomaji na kijitambua, na kutumia wakati kwa mambo yenye manufaa pamoja na kujenga kujiamini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: