Kuanza hatua ya kwanza ya kukarabati mlango wa Imamu Ali Haadi (a.s) kwa ndani

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandosi katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesema kuwa wameanza kukarabati mlango wa Imamu Ali Haadi (a.s), uliopo upande wa kaskazini mashariki ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ndani, na kuishia katika mlango wa zamani unao angaliana na ukumbi wa haram tukufu.

Akaongeza kuwa: “Hatua ya kazi za mradi huu zimegawanywa kutokana na milango, tulianzia katika mlango wa Imamu Mussa bun Jafari (a.s) uliopo mashariki magharibi ya ukumbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), tumeendelea hadi kwenye mlango huu, tutaandaa usanifu maalum kwa kila mlango wa haram tukufu, ambayo ipo milango tisa, kwa namna ambayo itaendana na muonekano wake wa nje pamoja na haram takatifu kwa ujumla, tunaanza kutoa vifaa vya zamani vilivyo tumika kujenga milango hiyo kutokana na kila mlango ulivyo pamoja na mpango wake wa kuukarabali chini ya kampuni inayo tekeleza mradi huo, ambayo ni kambuni ya ujenzi wa ardhi takatifu”.

Kumbuka kuwa haram na ukumbi wa Ahulfadhil Abbasi (a.s), vimeshuhudia miradi mingi, kila mradi unavipengele vyake maalum, kama vile mradi wa upanuzi wa jengo, mradi wa upauwaji, mradi wa kuweka marumaru, mradi wa kutengeneza dirisha takatifu, uwekaji wa mifumo mbalimbali, kama vie mfumo wa viyoyozi, zima moto, tahadhari, mawasiliano, ulinzi na miradi mingine nafasi haitoshi kuitaja yote, ndio tunaendelea na mradi huu ambao ni muhimu sawa na miradi iliyo tangulia, nao ni mradi wa kukarabati milango ya malalo tukufu kwa ndani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: