Chuo kikuu cha Al-Ameed kinafanya majlisi ya kukumbuka kifo cha Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake (r.a) ambayo ndio mazingira tunayo ishi katika siku hizi.

Majlisi hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), kwa kufuata maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na muongozo wa idara ya afya, unaosisitiza kuwepo kwa umbali fulani kati ya mtum na mtu na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi katika majlisi za uombolezaji, imehudhuriwa na wakufunzi wa chuo pamoja na wakuu wa vitengo na watumishi wake, na rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali na makamo wake.

Baada ya kusomwa Quráni tukufu na wimbo wa Atabatu Abbasiyya (Lahnul-Iba) pamoja na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kulikuwa na muhadhara uliotolewa na Sayyid Adnani Jalukhani Mussawi kutoka kitengo cha Dini katika Ataba takatifu, amezungumza mambo mbalimbali kuhusu harakati ya bwana wa mashahidi (a.s) na historia yake tukufu, pamoja na mafanikio yaliyo patikana kutokana na damu yake takatifu iliyo mwagika katika ardhi ya Karbala.

Na namna alivyo fanikiwa kubadilisha hali ya wakati ule pamoja na idadi chache ya watu aliokuwa nao, akapata ushindi ambao bado athari yake inaendelea hadi sasa, na amekuwa taa linalo angaza kila zama na muongozo wa kila mtu hudu duniani, akamaliza muhadhara wake kwa kueleza namna alivyo uwawa (a.s) na kutekwa familia yake.

Majlisi ikahitimishwa kwa beti za tenzi zilizo somwa na Muhammad Usfuur zilizo amsha huzuni kuhusu kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: