Makumbusho ya Alkafeel yanahifadhi dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) lililotengenezwa zaidi ya miaka 250 iliyopita.

Maoni katika picha
Mtu anaetembelea makumbusho ya malikale na nakala kale ataona vifaa vyenye mamia ya miaka, miongoni mwa vifaa hivyo ni dirisha lililokuwa juu ya kaburi tukufu la Abulfadhil Abbasi (a.s) mwaka 1182 hijiriyya, nalo ni miongoni mwa madirisha adimu na lenye thamani kubwa, limetengenezwa kwa ufundi wa hali ya juu na umaridadi mkubwa, limekuwepo katika miongo muhimu ya harakati za ujenzi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa makumbusho Ustadh Swadiq Laazim, dirisha hilo lilitengenezwa kwa ufundi mkubwa na umaridadi wa hali ya juu katika zama ambazo hakukuwa na teknolojia, hivyo lilitengenezwa kwa mikono, nalo ni dirisha adimu na lenye thamani kubwa, hiyo ndio sifa ya madirisha yote yaliyo wahi kuwekwa katika malalo hii, kutokana na umuhimu wa dirisha hilo, imeandaliwa sehemu maalum kwa ajili yake inayo endana na ukubwa wake”.

Akaongeza kuwa: “Tumefanya marekebisho baadhi ya sehemu za dirisha hilo na kuliweka katika makumbusho”.

Kumbuka kuwa dirisha lililopo hivi sasa katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) lilitengenezwa katika kiwanda cha Saqaa cha utengenezaji wa madirisha ya juweka juu ya makaburi na mazaru tukufu kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, nalo ni dirisha la kwanza la aina hiyo kutengenezwa hapa Iraq chini ya mafundi wazalendo miongoni mwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), dirisha hilo linaubora wa ziyada ikiwa ni pamoja na uzuri wa nakshi na mapambo yake, liko tofauti na madirisha yaliyopo kwenye malalo zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: