Kamati ya maamndalizi ya shindano la kaswida Aljuud na semi za Almujtaba (a.s), imetangaza kuahirisha mashindano hayo mwaka huu, kutokana na kuheshimu maagizo ya kujikinga na maambukizi ya virusu vya Korona yanayo sisitiza umbali kati ya mtu na mtu na kujiepusha na mikusanyiko.
Shindano la Aljuud lilikuwa lifanyike mwezi (13 Jamadal-Aakhar 1442h) na shindano la semi za Mujtaba (a.s) mwezi (4 Safar 1442h) yameahirishwa hadi mwaka kesho tarehe itapangwa na kamati husika siku za mbele.