Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kinaendelea na program ya kupuliza dawa katika mkoa wa Basra.

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdu-Shaábi) kinaendelea na opresheni ya kupuliza dawa kwenye mikoa tofauti hapa Iraq, hivi karibuni kimepuliza dawa katika mkoa wa Basra pamoja na Maahadi ya taaluma na chuo kikuu cha teknolojia cha kusini.

Msemaji wa kikosi ameripoti kuwa: opresheni hii imehusisha Maahadi ya taaluma na chuo kikuu cha teknolojia cha kusini ya Basra, kutokana na kumbi zake kutumiwa katika mitihani ya wanafunzi wa darasa la sita.

Akaongeza kuwa: Opresheni hii inafanywa kwa kushirikiana na kamati ya kupambana na maambukizi ya mkoa wa Basra.

Msemaji wa kamati hiyo amepongeza kazi nzuri inayo fanywa na kikosi cha Abbasi inayo pelekea kufanikisha ufanyaji wa mitihani ya mwaka huu, kwa kupuliza dawa za kujikinga na maambukizi ndani ya kumbi za mitihani mfululizo.

Kumbuka kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) kiliunda kamati maaluma ya kupambana na maambukizi ya Korona mwanzoni kabisa baada ya kutokea janga hilo, kamati hiyo imepuliza dawa sehemu mbalimbali, hasa zinazo kaliwa na watu, na inafanya kila iwezalo kupambana na janga hili, aidha imejenga kituo cha kuosha, kuvusha sanda na kuzika watu waliokufa kwa maradhi ya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: