Kitengo cha uhandisi wa majengo kimemaliza hatua ya pili ya kukarabati baadhi ya sehemu za hospitali ya watoto ya Karbala

Maoni katika picha
Kitengo cha uhandisi wa majengo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimemaliza hatua ya pili ya kukarabati baadhi ya sehemu za hospitali ya watoto ya Karbala, ukarabati huo umekamilika pamoja na kuwa na majukumu ya nje kama vile ujenzi wa vituo vya Alhayaat kwa ajili ya kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona kwenye mikoa tofauti, na kazi za ndani zinazo husu Ataba tukufu.

Kiongozi wa kazi za majengo ya kihandisi Muhammad Mustwafa Twawiil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hatua hii ni sehemu ya kukamilisha hatua iliyopita, iliyo husisha ukarabati wa vyoo vya hospitali, vilivyo kuwa vimeharibika na kuchakaa, eneo la vyoo linaukubwa wa mita (18) na kunavyoo sita na sehemu ya kunawa mikono, tumekarabati na kuweka vifaa vya kisasa”.

Akasema: “Vyoo hivyo vimefanyiwa matengenezo makubwa, vimejengwa upya kila sehemu, tumeondoa sakafu ya zamani na kuweka mpya, pamoja na kuweka vazi jipya la ukuta pamoja na dari, tumefunga taa mpya na mitambo ya kutoa hewa chafu, tumeweka hita za kuchemsha maji, tumefunga milango mipya, na kufanya matengenezo ya muonekano wa nje sambamba na kuweka viti vipya na kujenga njia mpya za maji taka”.

Kumbuka kuwa kazi za kukarabati hospitali hii ni sehemu ya shughuli za kibinaadamu zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na inaingia katika mkakati wa kukarabati majengo ya serikali yaliyopo katika hali mbaya, tumesha fanya hivyo kwenye shule na taasisi za kibinaadamu kama vile Darul-Hanaan ya watu wenye matatizo ya akili na sehemu zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: