Marjaa Dini mkuu amesema kuwa: Uchaguzi wa mapema sio lengo peke yake, bali ni njia sahihi ya kutoka katika hali ya sasa na kuchelewa kufanya uchaguzi kutaongeza matatizo

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesema kuwa kufanya uchaguzi wa mapema sio lengo peke yake, bali ni njia sahihi ya kuondoka katika hali inayo likumba taifa kwa sasa, katika sekta ya siasa, uchumi, amani, afya nk.. lazima wananchi wapewe nafasi ya kuchagua bunge lijalo kwa uhuru na amani, bila kushurutishwa na yeyote, kuchelewa kufanya uchaguzi kutaongeza matatizo ya nchi na kutishia umoja wa taifa na mustakbali wake.

Ameyasema hayo siku ya Jumapili mwezi (24 Muharam 1442h) sawa na tarehe (13 Septemba 2020m) alipokutana na Jenin Haines, muwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa hapa Iraq, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

Kufanya uchaguzi wa mapema sio lengo peke yake, bali ni njia sahihi ya kuondoka katika hali inayo likumba taifa kwa sasa, katika sekta ya siasa, uchumi, amani, afya nk.. lazima wananchi wapewe nafasi ya kuchagua bunge lijalo kwa uhuru na amani, bila kushurutishwa na yeyote, na bunge hilo litatue matatizo ya wananchi. Kuendelea kuchelewa kufanya uchaguzi au kufanya bila kufuata taratibu za uchaguzi huru na wa haki, kwa namna ambayo matokeo yake hayatakubaliwa na sehemu kubwa ya raia kutaongeza matatizo ya taifa –Allah atuepushie- na kutishia mustakbali wa nchi, kila mtu atajuta mambo yatakapo haribika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: