Marjaa Dini mkuu amesema: Serikali iliyopo inatakiwa kuendeleza utulivu na kufanya uadilifu

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesema: serikali iliyopo inatakiwa kuendeleza utulivu na kufanya uadilifu, pamoja na kulinda mipaka na kuboresha vyombo vya ulinzi na usalama, sambamba na kuchukua siraha ambazo zipo mikononi mwa watu kinyume na sheria.

Ameyasema hayo siku ya Jumapili mwezi (24 Muharam 1442h) sawa na tarehe (13 Septemba 2020m) alipokutana na Jenin Haines, muwakilishi maalum wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa hapa Iraq, lifuatalo ni tamko kuhusu swala hilo:

Hakika serikali iliyopo inatakiwa kuendeleza utulivu na kufanya uadilifu, pamoja na kulinda mipaka na kuboresha vyombo vya ulinzi na usalama, sambamba na kuchukua siraha ambazo zipo mikononi mwa watu kinyume na sheria, wala isikubali baadhi ya maeneo kutawaliwa na makundi yenye siraha kwa mtutu wa bunduki chini ya visingizio mbalimbali kinyume na sheria.

Serikali inatakiwa kuchukua hatua madhubuti za kupambana na ufisadi kwa mujibu wa sheria, kila mtu aliye fanya ufisadi ahukumiwe kisheria na arudishe mali za wananchi bila kujali nafasi yake au chama chake.

Aidha inawajibika kumchukulia hatua kila aliyeshiriki katika jinai ya kuuwa au kujeruhi au kufanya shambulio lolote kwa waandamanaji au vyombo vya ulinzi na usalama, au aliharibu mali za umma au binafsi, tangu lilipo anza vuguvugu la kudai mabadiliko (islahi) mwaka jana, hususan wale waliofanya vitendo vya utekaji na mashambulio mengine.

Hakika kuwachukulia hatua watu waliofanya makosa tuliyo taja ni jambo linalotakiwa kufanyika siku yeyote, ni njia sahihi ya kuzuwia jambo hilo lisirudiwe tena na kuogopesha watu wengine kufanya hivyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: